Bomu hilo lililokuwa la kutegwa kando ya barabara limewauwa wanajeshi watatu wa serikali ya mpito ya Somalia pamoja na raia mmoja huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika mkasa huo.Bomu hilo la kutegwa kando ya barabara limetajwa kuwani shambulio la wanamgambo wa ash Shabab wanaondesha vita dhidi ya serikali ya mpito ya Somalia. Wakati huo huo, mashambulio ya kigaidi ya ndege zisizo na rubani za Marekani yamezidi kuteketeza roho za raia nchini Somalia. Watu wengine 14 wameripotiwa kuuawa kusini mwa Somalia katika eneo linalopakana na Kenya baada ya ndege za Marekani zisizo na rubani kufanya mashambulio katika eneo hilo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 280541
Hali ya machafuko imeendelea kutawala nchini Somalia baada ya watu wengine wanne kupoteza maisha yao kufuatia mlipuko wa bomu katika mji mkuu Mogadishu.